Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
UIDHINISHAJI WA MIKOPO

  • 1. LULU SACCOS haitatoa mkopo bila idhini ya kamati ya mkopo
  • 2. Kamati ya mikopo haitaidhinisha mkopo kama sehemu ya mkopo haijadhaminiwa au mkopo haujadhaminiwa kikamilifu
  • 3. Kamati ya mkopo itaridhia ombi la mkopaji kupewa mkopo baada ya kujiridhisha na uwezo wa mwanachama kufanya marejesho.
  • 4. Kupatiwa/ kulipwa mkopo kwa mkopaji kutafanywa na chama kwa njia ya fedha taslimu kupitia katika ofisi za chama, au kwa kupitia katika akaunti zao za wateja zilizopo katika benki washirika au kuhamishiwa kwenye akaunti ya mkopaji baada ya kukamilika kusainiwa kwenye mkataba wa mkopo huo.Na mkopaji anaweza kuweka fedha zake kwenye akaunti yake ya amana iliyopo katika chama wakati anasubiria kufanya malipo ya bidhaa/huduma anayoilipia.
  • 5. Kamati ya mikopo ina haki ya kukataa/kukubali au kupunguza kiwango cha mkopo. Uamuzi wa kurudisha maombi ya mkopo utatolewa na Bodi na sio kamati ya mikopo kwa mwanachama ikiwa mwanachama atakuwa hakutimiza vigezo vya kupewa mkopo kama ilivyoelekezwa katika sehemu ya 2.1 ya sera hii.
  • 7. Ikiwa ombi la mkopo halijakubaliwa LULU SACCOS itamfahamisha mwanachama sababu za kukatatiliwa kwa ombi lake ndani ya kipindi cha siku saba.
  • 8. Fedha za mikopo zitatolewa kutegemeana na hali ya ukwasi chamani lakini kwa namna yeyote ile mikopo midogo itapewa kipaumbele ikiwa hali ya ukwasi wa chama iko chini.
  • 9. Kamati ya mikopo haitaidhinisha kiwango cha mikopo kinachoanzia shilingi 100,000,000 na kuendelea
  • 10.Kamati ya kitaalamu haitaidhinisha kiasi cha mikopo kinachozidi shillingi 4,000,000/=
  • 11. Kiasi cha mkopo kinachoanzia shilingi 100,000,000/= na kuendelea kitaamuliwa na kuidhinishwa na Bodi ya chama
  • 12. Kamati ya mikopo/kamati ya kitaalam na Bodi itatumia kumbukumbu zifuatazo ili kufikia uamuzi wake;
  • Mali anazotumia mwanachama kudhamini mkopo
  • Daftari linaloonyesha orodha ya wanachama
  • Uzoefu katika shughuli anayoombea mkopo
  • Aina ya mradi unaoombewa mkopo
  • Mahali mradi ulipo Pamoja na vigezo vingine vitakavyowekwa na chama.
  • Kanuni ya 30 ya kanuni za huduma ndogo za fedha za mwaka 2019
  • News 1
    Karibu Sana

    Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

    picture-ya-Pesa
    Vyanzo vya Mapato

    • (a) Hisa za wanachama
    • (b) Malimbikizo ya faida
    • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
    • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
    • (e) Akiba za wanachama
    • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

    Ufahamu Zaidi

    BIMA YA MIKOPO

    Mkopo ni chachu ya maendeleo na husaidia...

    Read More
    DHAMANA YA MKOPO

    Wadhamini wa mkopo watawajibika moja kwa moja...

    Read More
    UIDHINISHAJI WA MIKOPO

    Uidhinishaji wa maombi ya mikopo.LULU SACCOS ha...

    Read More