Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
DHAMANA YA MKOPO

  • 1. Wadhamini wa mkopo watawajibika moja kwa moja endapo mkopo uliodhaminiwa utashindwa kurejeshwa kwa kipindi kilichokubaliwa katika mkataba wa mkopo.Wadhamini watapaswa kuwajibika kulipa mkopo mara baada ya mkopaji kushindwa kurejesha mkopo kwa utaratibu uliokubalika na kwa kutumia dhamana zake.
  • 2. Dhamana mali zitahakikiwa na kuwa chini ya ulinzi wa Chama au wadhamini kwa kipindi chote cha mkopo.
  • 3. Sehemu ya amana inayodhaminiwa haitachukuliwa mpaka mwanachama amemaliza kurejesha mkopo na kama hatarejesha ndani ya siku saba amana yake itakatwa kulipia rejesho.
  • 4. Akiba, hisa, na Amana za wadhamini zitachukuliwa na chama ikiwa aliyewekewa dhamana atashindwa kurejesha mkopo baada ya mkataba kuisha.
  • 5. Taarifa ya maandishi itapelekwa kwa wadhamini kwa kusudio la kuchukua Akiba, Hisa, au Amana zao ndani ya siku saba baada ya mkataba wa mkopo kuisha.
  • 6. Chama kitakuwa na haki ya kuuza dhamana iliyowekwa ili kufidia deni.
  • 7. Dhamana zote zitadhamini mkopo husika hadi deni litakapokamilika kulipwa.
  • 8. Mdhamini atakuwa ni yule tu mwanachama wa LULU SACCOS LTD ambaye ana Hisa zisizopungua 100 na kuendelea. Mdhamini wa mkopo wowote atatakiwa kuwa amekuwa mwanachana kwa zaidi miezi 12, pia kamati itazingia hali ya mdhamini.
  • 9. Mwanachama anayedaiwa rejesho au marejesho hatoruhusiwa kuchukua amana zake. Afisa mikopo atatoa taarifa kwa Meneja kuhusiana na marejesho ya wadaiwa ili fedha zikatwe kwenye akaunti zao za amana.
  • 10. Haki ya kukamatwa mali yoyote ya mkopaji tofauti na mali iliyowekwa dhamana.
  • Mkopeshaji atakuwa na haki ya kutekeleza dai la haki (bonafide claim of right) kwa mujibu wa sheria za nchi katika kuhakikisha kuwa MKOPAJI anarejesha deni kwa MKOPESHAJI. Hivyo basi MKOPESHAJI atakuwa na haki ya kukamata mali yoyote ya MKOPAJI nje ya mali aliyoweka dhamana endapo lolote kati ya mambo yafuatayo yatatokea;
  • Mkopeshaji atakuwa na haki ya kukamata mali ya mwenza wake (mke/mume) msimamizi au mrithi wa mirathi aliyesaini fomu ya mkataba kama juhudi nyingine zote za kukombolea deni lote zimeshindikana.
  • Kama dhamana ya mkopaji imeuzwa na haikuweza kufidia deni lote.
  • Pale ambapo imejulikana kuwa mkopaji amefanya udanganyifu wa aina yoyote ili kujipatia mkopo.
  • Kama mkopaji amehukumiwa kwa kosa lolote la jinai na kuonekana kuwa hana uwezo wa kulipa mkopo.
  • Kama mkopaji atatenda jambo lolote ambalo ni kinyume na maadili ya nchi kinyume na matarajio ya umma (acts against morals and public interest).
  • Kama mkopaji atafukuzwa uanachama kwa mujibu wa sheria, kanuni na masharti ya chama.
  • Kama itabainika kuwa mkopaji anataka kutoroka na kwenda nje ya nchi kwa sababu yoyote ile.
  • Kama mkopaji atatangazwa kufilisika.
  • News 1
    Karibu Sana

    Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

    picture-ya-Pesa
    Vyanzo vya Mapato

    • (a) Hisa za wanachama
    • (b) Malimbikizo ya faida
    • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
    • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
    • (e) Akiba za wanachama
    • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

    Ufahamu Zaidi

    BIMA YA MIKOPO

    Mkopo ni chachu ya maendeleo na husaidia...

    Read More
    DHAMANA YA MKOPO

    Wadhamini wa mkopo watawajibika moja kwa moja...

    Read More
    UIDHINISHAJI WA MIKOPO

    Uidhinishaji wa maombi ya mikopo.LULU SACCOS ha...

    Read More