Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
MKOPO WA KILIMO NA UNUNZI WA MAZAO

Mkopo huu utatolewa kwa awamu tatu ambazo ni mwezi wa nne, mwezi wa saba na mwezi wa kumi. Pia Mkopo huu umegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni:-

  • 1. MKOPO WA UNUNUZI WA MAZAO YA NAFAKA
  • Wanachama wanaokusudiwa ni wale wanaofanya biashara ya kununua mazao wakati wa mavuno kwa ajili ya kuyauza wakati wa baadae. Mazao yanayopendekezwa na Bodi ni kama mpunga, ngano, karanga, maharage, alizeti na ulezi.
  • 2. MKOPO WA UNUNUZI WA MAZAO YA MISITU
  • Mkopo huu unawalenga wafanyabiashara wa misitu wenye vibali na usajili halali wa kufanya biashara hiyo. Mfano wa mazao ya misitu yanayopendekezwa na bodi ni asali, nta, kuni, mbao na mkaa.

  • Taratibu za utoaji wa mikopo ya ununuzi wa mazao ya nafaka na misitu
  • a. Mkopaji atajaza fomu maalumu ya kuomba mkoo huu
  • b. Muda wa mkopo huu ni miezi mitano au miezi kumi na moja (11) na kwamba marejesho ya mkopo huu lazima yafanyike ndani ya miezi mitatu ya mwisho toka tarehe na mwezi wa kupewa mkopo huu kwa mkopo wa miezi 11 na yatafanyika kwa muda wa miezi miwili ya mwisho kwa mkopo wa miezi mitano.
  • c. Tozo la riba ni 7.5% au 15% kutegemeana na muda wa mkopo
  • d. Kiasi cha chini cha mkopo wa ununuzi wa mazao ni Tshs.5, 000,000/= (milioni tano)
  • e. Kiasi cha juu cha mkopo wa ununuzi wa mazao ni Tshs.200, 000,000/= (milioni mia moja na hamsini tu)
  • f. Pamoja na taratibu za mikopo na dhamana zilizoainishwa kwenye sera yetu ya mikopo, mwombaji wa mkopo huu atawajibika au atapaswa kuwasilisha mchanganuo wa zao analotaka kununua ikiwa ni pamoja na kuishawishi Bodi juu ya uzoefu wake katika kufanya biashara hiyo na uhakika wa marejesho yake
  • g. Mwombaji atakayepata mkopo huu atalazimika kulipia bima ya maisha ya mkopo ya asilimia 0.8%
  • h. Afisa mikopo pamoja na kamati ya mikopo watayafanyia kazi maombi ya waombaji wote wa mikopo ya mazao kwa wakati na kutoa taarifa rasmi ya maandishi ya lini wakopaji watapewa mikopo. Mikopo itatolewa baada ya taratibu zote za awali kukamilika Pia mkataba wa mkopo huu utathibitishwa na Mwanasheria.
  • i. Mwanachama anayeruhusiwa kukopa mkopo huu ni yule aliyejiunga zaidi ya mwaka mmoja ndani ya ushirika huu.
  • j. Mkopaji atawajibika kuwa na kiasi cha hisa zinazowiana na viwango vilivyowekwa kwa viwango mbalimbali vya mikopo.
  • k. Mikopo ya mazao itajadiliwa na kuidhinishwa na bodi ya LULU SACCOS
  • l. Mkopaji atajaza mkataba wa mkopo

News 1
Karibu Sana

Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

picture-ya-Pesa
Vyanzo vya Mapato

  • (a) Hisa za wanachama
  • (b) Malimbikizo ya faida
  • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
  • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
  • (e) Akiba za wanachama
  • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

Ufahamu Zaidi

BIMA YA MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More
USIMAMISHAJI MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More
UREJESHAJI WA MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More