Utaratibu wa Mikopo

Mikopo hutolewa kwa mwanachama na wafanyakazi wa Lulu Saccos. Mkopaji atajaza fomu ya mikopo na atatoa mchanganuo wa mkopo, mfan...

Read More
MKOPO WA BIASHARA

Mkopo huu unalengo la kumsaidia mwanachama, kikundi au mkopaji kuendesha shughuli zake za biashara kwa kuongezea mtaji na hivyo kuleta kasi ya mzunguko wa biashara yake na kukabiliana na ushindani wa kibiashara kwa riba nafuu.

    KAMATI YA MIKOPO ITAZINGATIA YAFUATAYO:

  • 1. Mkopo wa biashara utakopeshwa kwa mwanachama ambaye tayari anayo biashara bila kujali biashara ni kubwa au ndogo ii. Riba ya mkopo huu ni 1.5% kwa mwezi
  • 2. Mwombaji atajaza fomu ya kuomba mkopo wa biashara na kuirudisha kwa Afisa mikopo ikiambatanishwa na mchanganuo ambao utaonyesha biashara anayofanya au anayokusudia kuifanya
  • 3. Kabla chama hakijatoa mkopo wa biashara Afisa mikopo au kamati ya mikopo itafika na kuona eneo la biashara ilipo au inapokusudiwa kuanzishwa.
  • 4. Mikopo ya biashara dhamana yake itakuwa, Hisa, Akiba, Amana ya Mwanachama, Mradi wenyewe kupitia biashara akaunti,na Hati mbalimbali za umiliki wa mali.
  • 5. Kiwango cha mkopo kitatakiwa kuwiana na viwango maalum vya Hisa vilivyowekwa.
  • 6. Mkopo wa biashara unaoanzia kiasi cha 100,000,000/=utajadiliwa na kuidhinishwa na Bodi ya chama.
  • 7. Kiwango cha juu cha mkopo huu ni shilingi 299,999,999/=
  • 8. Mwanachama hataruhusiwa kukopa mkopo huu wa biashara endapo hatarejesha mkopo wa dharura.
  • 9. Muda wa mkopo huu ni kuanzia miezi 3, 6, 12, 18, 24 na 36 na marejesho yake ni kila mwezi.
  • 10. Mwombaji atajaza mkataba wa mkopo.
News 1
Karibu Sana

Lulu Saccos tupo Soweto Mbeya Mjini, tunatazamana na barabara kuu ya Tanzania Zambia

picture-ya-Pesa
Vyanzo vya Mapato

  • (a) Hisa za wanachama
  • (b) Malimbikizo ya faida
  • (c) Mikopo kutoka taasisi mbalimbali za kifedha na zisizo za kifedha
  • (d) Misaada kutoka kwa wafadhili wa ndani na nje ya nchi
  • (e) Akiba za wanachama
  • (f) Uwekezaji wa wanachama na wadau mbalimbali

Ufahamu Zaidi

BIMA YA MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More
USIMAMISHAJI MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More
UREJESHAJI WA MIKOPO

Brief description of the news or event.

Read More