MKOPO MAALUM WA BIASHARA (COMMERCIAL SPECIAL LOAN)
Mkopo huu unalenga kumsaidia Mwanachama au asasi zingine za kifedha kuendesha shughuli zake za biashara kwa kumuongezea mtaji na hivyo kuleta kasi ya mzunguko wa biashara yake na kukabiliana na ushindani wa biashara kwa riba nafuu.
Mkopo huu una masharti yanayofanana na mkopo wa biashara lakini wenyewe kiwango chake ni kuanzia milioni mia tatu (300,000,000/=) na kiwango cha juu ni milioni mia sita (600,000,000/=)
Mkopo maalum utakopeshwa kwa mwanachama ambaye tayari ana biashara inayowiana na kiasi cha mkopo kinachoombwa.
Mkopaji atajaza fomu maalumu ya mkopo
Kabla chama hakijatoa mkopo maalumu afisa mikopo, meneja au kamati ya mikopo itafika ili kuona na kukagua biashara ili kujiridhisha na uwezo wa biashara inayoombewa mkopo huo.
Dhamana za mkopo maalumu zitakuwa ni pamoja na
a. Hisa, Akiba, Amana ya mwanachama
b. Hati mbalimbali za mali zisizohamishika
Riba yake itakuwa asilimia 1.5%
Mkopo huu utakopeshwa kwa muda wa miezi sita hadi Arobaini na nane (48)
Kiwango cha mkopo huu kitakuwa mara moja, mbili au tatu ya akiba za Mwanachama
Kiwango cha mkopo kitatakiwa kuwiana na viwango maalumu ya hisa vilivyowekwa na chama.
Mwanachama hataruhusiwa kuwa na mkopo wa biashara pamoja na mkopo maalum wa biashara kwa wakati mmoja.
Mwanachama hataruhusiwa kukopa mkopo maalum endapo hajarejesha mkopo wa dharura
Mwanachama anayeruhusiwa kukopa mkopo huu ni yule aliyejiunga zaidi ya mwaka mmoja ndani ya ushirika wa LULU SACCOS
Mwombaji atakayekuwa na sifa za kupata mkopo huu atapewa mkataba na kuujaza.
Maombi yote ya Mkopo maalum yatajadiliwa na Kamati ya Mikopo, na kuidhinishwa na Bodi ya LULU SACCOS.